Habari

Ni Majanga kwa Mary J. Blige: ‘No Money, Mo Problems’

The Queen of Soul, Mary Jane Blige yuko katika wakati mgumu aki-experience ‘remix’ ya ule msemo wa ‘MO Money Mo problems’ ambao kwake ni kinyume chake ‘No Money Mo problems’.

Mary-J-Blige-Broke

MJB mwenye miaka 42 sasa anaukwea uzee vibaya kutokana na hali mbaya ya maisha aliyonayo sasa inayotokana na kuyumba kiuchumi na kuzungukwa na madeni yanayofikia dola million 3.4.

Majanga ya kiuchumi yamemwandama MJB kwa miaka mingi sasa ambapo mwaka jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya charity organization aliyoianzisha FFAWN (Foundation For The Advancement Of Women Now, Inc.) kushindwa kurudisha mikopo. Baadae kuliibuka uvumi kuwa Mary J ameshindwa kulipa kodi ya nyumba huko New York, na sasa jumla ana deni kubwa la dola million 3.4

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents