Habari

Ni mwizi kama wezi wengine, tofari elfu 5, namvua madaraka hapa hapa – Naibu Waziri Silinde (+Video)

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. David Silinde amemkabidhi Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Ikhanoda Kata ya Ikhanoda iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Singida Omary Selestine  kwa jeshi la Polisi na TAKUKURU baada ya kugundua matumizi mabaya ya fedha za umma  katika ujenzi wa bwalo la chakula kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.

Hatua hiyo imetokea baada ya Mhe. Silinde kufanya ziara katika shule hiyo kukagua mradi wa lipa kutokana matokeo (EP4R) ambao shule hiyo walipewa kwa ajili ya ujenzi wa bwalo lakini mpaka sasa fedha zaidi ya milion 50 zimetumika huku ujenzi ukiwa  katika hatua ya msingi hali iliyopelekea naibu waziri kuona kuna ubadhitifu mkubwa wa fedha huku baadhi ya vifaa vikinunuliwa kwa bei ya juu sana kuliko uhalisia wa bei.

“Huwezi nunua mabati ya milioni 70 unataka kujenga nini,au unanunua tofali kwa shilingi elfu tano ni tofali aina gani,Kamanda wa Polisi na TAKUKURU mchukue huyu mwalimu na kamati nzima ya ujenzi wakaeleze wametumiaje fedha za ujenzi wa mradi huu ” Alisema Mhe. Silinde

Katika hatua nyingine Mhe. Silinde amemsimamisha kazi mwalimkuu huyo na kuvunja kamati ya ujenzi ya shule hiyo na kumvua madaraka afisa mtendaji wa Kata hiyo baada ya kushindwa kusimamia ujenzi wa bwalo la chakula katika shule hiyo.

Aidha Afisa Mtendaji wa Kata hiyo ametuhumiwa  kuhusika moja kwa moja katika ubadhilifu huo na kuagiza jeshi la polisi pamoja na Takukuru kufanya uchunguzi wa kina na kupelekewa ripoti yote fedha zilivyotumika vibaya.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Singida Mhe. Pascas Muragili amesema kamati ya Ulinzi na Usalama  ya wilaya walituma Takukuru kuchunguza ujenzi huo na kubaini kuwa kuna ubadhilifu wa fedha katika mradi huo nakutoa mapendekezo kwa mkurugenzi kumsimamisha kazi mwalimu huyo.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Omary Selestine amesema mpaka sasa wameshatumia milion 57.6 kati ya milion 100 walizopewa kwa kununua vifaa vyote vya ujenzi kasoro mabati na wanategemea ujenzi huo ukamilike mwishoni mwa mwezi wa huu kwanza.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents