Michezo

Ni vita ya Andy Murray na Stan Wawrinka French Open

Mchezaji namba moja katika viwango vya ubora wa mchezo wa Tenisi duniani, Andy Murray anaamini anakabiliwa na kibarua kizito dhidi ya mpinzani wake Stan Wawrinka katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya Ufaransa kuwania tiketi ya kucheza hatua ya fainali.

Mchezaji namba moja katika viwango vya ubora wa mchezo wa Tenisi duniani, Andy Murray

Murray ambaye anafanya kazi peke yake ameonekana kuwepo katika kiwango bora tangu alipopata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Andrey Kuznetsov, lakini pia akishinda dhidi ya wachezaji Martin Klizan, Juan Martin del Potro, Karen Khachanov pamoja na Kei Nishikori.

Mcheza tenisi Andy Murray (kulia)  na Stan Wawrinka (kushoto)

Kwa kupata matokeo hayo kunamfanya kuwa katika kiwango bora zaidi cha kukabiliana na bingwa huyo wa michuano ya Switzerland Davis Cup mwaka 2015 , Wawrinka mchezo utakaopigwa ijumaa.

Wakati Bingwa mara tisa wa michuano ya wazi ya Ufaransa, Rafael Nadal yeye atakuwa na kibarua kizito atakapo mkabili mchezaji Dominic Thiem katika nusu fainali ya pili mchezo utakaopigwa huko Roland Garros.

Mchezaji tenisi, Rafael Nadal (kushoto) na Dominic Thiem(kulia)

BY  HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents