Michezo

Ni vita ya miamba miwili nusu fainali klabu bingwa Ulaya

Michuano ya klabu bingwa barani Ulaya inatarajiwa kuendelea hii leo siku ya Jumanne kwa mchezo wa kwanza wa nusu fainali kupigwa dimba la Anfield ambapo Klabu ya Liverpool itakuwa mwenyeji dhidi ya AS Roma.

Liverpool wametinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa kabisa kwa ngazi ya klabu baada ya kuing’oa Manchester City kwa jumla ya mabao 5-1.
Wakati wapinzani wao klabu ya AS Roma nao hawakupata bahati ya mtende kuingia kwenye hatua hiyo bali walilazimika kupindua matokeo mbele ya wafalme wa soka wa Hispania, FC Barcelona na kuwatoa kwa faida ya bao la ugenini.
 Rekodi ya Liverpool na AS Roma kabla ya kukutana kwenye mchezo wao wa leo wa klabu bingwa Ulaya.

Mchezo mwengine wa klabu bingwa Ulaya unatarajiwa kupigwa kesho siku ya Jumatano wakati Bayern Munich ikiwakaribisha Real Madrid ya Hispania.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents