Habari

Ni vyakula gani vinavyoweza kuimarisha tendo la ndoa?

Kama kungekuwa na ushahidi kwamba chakula cha aina moja kinaweza kuimarisha tendo la ndoa na kukuzidishia hamu, huenda kungekuwa na uhaba wa chakula hicho.

A couple enjoying a romantic dinner on the beach

Lishe bora, kufanya mazoezi na afya nzuri ya akili yote yanaweza kuimarisha tendo la ndoa.

Lakini kuna vyakula vyovyote maalum vinavyoweza kukuongezea hamu ya tendo la ndoa ?

Viungo vinavyoweza kuchochea hisia ya furaha- kutokana na homoni ya endorphins, vina virutubisho vinavyohusishwa na kuimarika kwa tendo la ndoa, au kwa jumla vinahusishwa na utajiri na ufanisi na mara nyingi hutajwa kuwa vichochezi vya kuimarisha tendo hilo la ndoa.

Hebu tutazame historia kidogo na sayansi iliomo kwenye fikra hizi na tutafakari iwapo vyakula hivi vinaweza kweli kuimarisha tendo la ndoa.

Manufaa ya kula chaza au kombe?Oyster on a heart-shaped board

Casanova, mpenzi maarufu katika historia inaarifiwa alikuwa anakula  chaza 50 wakati wa kiamsha kinywa.

Hatahivyo hakuna uthibitisho baina ya kula chaza na kuongezeka kwa tendo la ndoa, basi uvumi ulitoka wapi?

Simulizi au ngano za kale zinaeleza kwamba wakati Aphrodite – Mungu wa tendo la mapenzi – alipozaliwa kutoka povu jeupe na kufufuka kutoka baharini ndipo chakula cha baharini kilipoonekana kuwa ni kichochezi cha kuimarisha tendo la ndoa.

Lakini kuna habari nzuri kwa wanaopenda kula chaza, wana madini ya zinc kirutubisho muhimu kinachotumika kuunda homoni ya testosterone.

Utafiti umebaini kwamba zinc inaweza kusaidia kutibu matatizo ya wanaume kuweza kuzalisha na huenda zinaweza kuongeza ubora wa manii.

Vyanzo vingine vizuri vya zinc hupatikana katika Nyama nyekundu, Mbegu kama za tango na sim simu, korosho na lozi lakini pia maziwa na hata jibini.

Chokoleti inaweza kukufanya mpenzi mzuri?A woman's lips biting a piece of chocolate

Kula chokoleti nyeusi kunaweza kukupa hisia ya awali unapompenda mtu, kwa mujibu wa utafiti, kwasbaabu ina ina ‘kemikali ya mapenzi’ phenylethylamine (PEA).

PEA – ambayo huwepo katika miezi ya kwanza ya mahusiano – huchangia kuwepo kwa homoni inayomfanya mtu kujihisi vizuri na kuchochea raha katikati mwa ubongo.

Ni kiwango kidogo tu cha PEA kipo katika chokoleti na kuna shaka iwapo kiwango hicho kinaendelea kuwepo wakati kinaliwa.

Cocoa pia ina amino acid tryptophan, na husemekana kuongeza msukumo wa damu na viwango vya serotonin (homoni nyingine ya furaha).

Basi uhusiano baina chokoleti na tendo la ndoa ulianza vipi? Huenda ni katika karne ya 16.

Hernán Cortés alikuwa mtawala wa Kihspania katika karne hiyo aliyeithibiti inayojulikana hii leo kama Mexico chini ya ufalme wa Castile.

Inadhaniwa ndio raia wa kwanza Ulaya kugundua chokoleti. Alimuandikia barua mfalme akimueleza kwamba amegundua kinyaji cha cocoa kinasaidia “kuimarisha kinga na kukabiliana na uchofu”.

Lakini raia wa zamani wa Castile huenda walihusisha nguvu hizo na chokoletina hakuna uhakikisho kuunga mkono ushahidi wa kuimarisha tendo la ndoa.

Pilipili kuchangamsha tendo la ndoa?A chilli pepperHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Pilipili zina kinachojulikana kama capsaicin, ambayo utafati umeaini inaweza kuchochea homoni ya endorphins (ya kujihisi furaha).

Husaidia pia kuharakisha ufanyaji kazi mfumo wa kusaga chakula tumboni na huongeza ujoto mwilini na kasi ya moyo unavyopiga, mambo ambayo huwa tunayahisi wakati wa tendo la ndoa.

Lakini hakikisha kwamba unakumbuka kuosha mkono unapotayarisha pilili!

Pombe husaidia au hutatiza?Two people's hands toasting with red wine

Pombe inaweza kuongeza hamu kwa kuondosha kujizuia, lakini kama anavyoeleza Macbeth wakati akiwa amelewa, “huchochea hamu, lakini huondosha uwezo”.

Hisia hupungua kwa wanaume na wanawake kwa kunywa pombe nyingi, na katika kipindi cha muda mrefu inaweza kupunguza uwezo wako wa kushiriki tendo la ndoa na hata mara nyingine katika hali mbaya zaidi kuchangia matatizo ya kushindwa kabisa kushiriki tendo hilo.

Zaidi ya hapo harufu ya pombe haivutii!

Vichochezi vya kuongeza hamuThe Birth of Venus by Sandro Botticelli (Italian, circa 1445 - 1510); tempera of canvas, circa 1486, from the Uffizi Gallery, Florence.

Aphrodite – Mungu wa tendo la mapenzi – alipozaliwa kutoka povu jeupe na kufufuka kutoka baharini ndipo chakula cha baharini kilipoonekana kuwa ni kichochezi cha kuimarisha tendo la ndoa

Vichochezi vinaweza kugawanywa katika makundi matatu.

Vinavyoshughulikia hamu, uwezo wa kushiriki tendo na raha inayotokana na tendo lenyewe.

Hakuna vilivyothibitishwa kisayansi kuwana uwezo wa kufanya kazi kwa binaadamu , kutokana na ugumu wa kupima ufanisi

Ni harufu ya kuiva na kuoza kwa tunda pekee ndiyo iliyoweza kuthibitishwa, na hufanya kazi kwa wadudu wa matunda wanaoruka.

Dr Krychman, mtaalamu wa afya ya ngono anasema anadhani watu hula vichochezi hivyo kwasababu ya imani kwamba vitafanya kazi, na anauliza iwapo jambo linakusaidia, je unajali kwanini inafanya kazi?

Vichochezi vingi huwa ni vinywaji, lakini imeshauriwa kuepuka dawa zinazotokana na mimea iwapo hazina taarifa ya usalama au yoyote inayotajwa kuwa ya miujiza.

Matatizo yaliopo

Iwapo hamu ya tendo la ndoa imepungua, huenda una tatizo la afya , kwa hivyo daima mshauri daktari.

Chanzo cha habari, shirika la habari BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents