Tia Kitu. Pata Vituuz!

Nick Minaj amnyamazisha Cardi B, Ndio Rapper wa kike mwenye mkwanja mrefu zaidi, Anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya kiasi hiki

Nick Minaj amnyamazisha Cardi B, Ndio Rapper wa kike mwenye mkwanja mrefu zaidi, Anakadiriwa kuwa na utajiri wenye thamani ya kiasi hiki

Nicki Minaj anafahamika ulimwenguni kama mmoja wa wanawake wenye ujuzi zaidi kuwahi kutokea katika muziki wa Hiphop. Siku hizi, amekuwa akishindanishwa zaidi na wasanii mbalimbali kuliko hapo awali lakini, kwa muongo mmoja uliopita, Minaj ametawala na amekuwa  Malkia wa hip-hop.

Ingawa bado anawika sana akiwa kama rapper mkali wa kike, licha ya nyota kama Cardi B na Megan Thee Stallion kumpa changamoto kwenye eneo hilo la kurap lakini Jambo moja ambalo anaweza kujivunia kuwa hawawezi na kuonesha kuwa bado ngumu madada hao wengine kumzidi ni ukweli kwamba rasmi Nick Minaj amekuwa Rapper wa kike mwenye mkwanja mrefu zaidi ukikadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 100 ambazo ni sawa na Bilioni 230 za Kitanzania, wamethibitisha Label ya Young Money kupitia twitter.

Fedha hizo zimetokana na mauzo ya kazi zake za muziki vile vile uwekezaji nje ya muziki.

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW