Burudani

Nicki Minaj amcheka Dj Khaled ‘He is crazy’ aijibu video aliyoombwa uchumba

Nicki Minaj na DJ Khaled kamwe hawawezi kuwa mtu na mke wake. Kwa mara ya kwanza Diva huyo wa Young Money amelijibu ombi la kuolewa na Dj Khaled.

634.minaj.mh.092812

Alimpigia simu Funkmaster Flex wa Hot 97 jana kuielezea video hiyo ya MTV News iliyomuonesha Khaled akielezea jinsi anavyompenda rapper huyo na pia kutoa pete ya thamani aliyopanga kumvisha.

“Nilishtuka kama dunia yote, nilikuwa nikicheka kama wengine Khaled ni master katika kile anachokifanya,”alisema Nicki.

KUMBE, Khaled alirekodi video hiyo kupigia promo single yake mpya kutoka kwenye albam yake mpya Suffering From Success, “I Wanna Be With You” aliyomshirikisha Nicki, Future, na Rick Ross.

“Ilikuwa ni njia nyingine ya yeye kuionjesha dunia feeling ya wimbo huo. Nobody in my real life took it seriously. Everybody just hit me like, ‘LOL. Yo, Khaled is crazy.”

Nicki aliamua kuzima matumaini yote ya kuwa mke wa Dj huyo kwa kudai kuwa ni kaka yake.

“Khaled is my brother and Khaled was not serious with that damn proposal, ya’ll. Please let it go. He was kidding. He’s not attracted to me, he doesn’t like me. We’re brother and sister.”

Licha ya Nicki kukataa, Khaled aliendelea kuwa serious na mpango hasa baada ya weekend hii kuongea kwa simu na DJ Felli Fel wa Power 106.

“She might say yeah tonight or tomorrow, she might say yeah next year. What am I gonna do, give up? Never. I ain’t never give up on nothing I do,” alisema.

Hata hivyo baada ya interview ya Nicki, Dj huyo alitweet: “Salute @NICKIMINAJ!!! … Bringing the excitement back to the game!”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents