Aisee DSTV!

Nicki Minaj amuita Rick Ross takataka asema ” Sitaki kumsikia mtu anayemtukana mwanamke ili auze album yake” – Video

Nicki Minaj amuita Rick Ross takataka asema " Sitaki kumsikia mtu anayemtukana mwanamke ili auze album yake" - Video

Swali lililoulizwa na Joe lilionekana kumkwanza mwanadada Nicki Minaj baada ya kumuuliza kwamba ni nani mkali kati ya The Game na Rick Ross? Majibu ya Minaj yalikuwa makali zaidi kwa Rozzy baada ya kusema kuwa:- “Hebu usiniletee hapa hiyo takataka, usinifanye nianze kumuongelea. Mtu yeyote anayemtukana mtoto wa Kike ili kuuza vinakala 250 vya album, usimlete kabisa mbele yangu. Hongera kwa The Game, anajua kuchana.” alizungumza Nicki.

Alienda mbali zaidi na kusema; Rozay hana fadhila kwa sababu alim-diss vibaya licha ya kuwahi kumsaidia msanii wake (Meek Mill) tena mbele ya Rais Obama kipindi wana mahusiano na alikuwa ameandamwa na matatizo ya kisheria.

“Nilienda kukutana na Obama, na Ross alikuwepo. Nilienda kuongea naye kuhusu masuala ya “Probation” baada ya kikao nilimuona Rozay akimtumia meseji Meek na kumuambia ‘Huyu mwanamke ni wa kumtunza sana’ Halafu leo unakuja kutoa Ki-album chako na kunitukana mimi, kalisha makalio yako manene huko” Alisema Minaj

By Ally juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW