Burudani

Nicki Minaj na Cardi B wamaliza tofauti zao ‘wote tumebarikiwa, sasa ni kazi tu’

Baada ya vuta nkuvute ya takribani miezi mitano kati ya Rappers wawiuli wa kike wanaofanya vizuri nchini Marekani Nicki Minaj na Cardi B, hatimaye wawili hao inaonekana kwa sasa wameamua kuweka pembeni taofauti zao.

Image result for cardi b MEETS nicki minaj
Nicki Minaj na Cardi B

Nicki Minaj ndiye aliyekuwa wa kwanza, ku-tweet kwenye ukurasa wake wa twitter kwa kuandika “Naomba kuanzia sasa tujikite kwenye vitu vya msingi, Wote tumebarikiwa. Najua haya mambo kuna watu wengi sana walikuwa wanafurahia lakini kwa sasa siwezi kuzungumzia upuuzi huo. Nashukuru sana kwa sapoti yenu ya mwaka hadi mwaka. Nawapenda.” .

Naye, Cardi B alichukua screenshot ya Tweet ya Nicki Minaj na kisha kuiposti kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika “sawa Nicki Minaj, kwa sasa tuanze kufanya kazi kwenda mbele“.

Nickiminaj alright then! Let’s keep it positive and keep it pushing!

 

Soma zaidi kuhusu bifu la Nicki Minaj na Cardi B – Hiki ndio kilichopelekea Nicki Minaj na Cardi B kutaka kudundana kwenye sherehe za Harper’s Bazaar ICONS

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents