Burudani

Nicki Minaj na Remy Ma uso kwa uso BET baada ya beef kali, nani zaidi?

Ni muda mrefu mashabiki wamekuwa wakikosa majibu ya kufahamu nani mkali kati ya Nicki Minaj na Remy Ma.

Wawili hao wamekuwa katika beef ya maneno tangu mwezi Disemba mwaka jana, baada ya Remy kuanza kumchana Nicki katika wimbo wake wa ‘SHETHER’ lakini alijibiwa na mrembo huyo wa Young Money alijibu mapigo kupitia nyimbo mbili alizoziachia mwezi Februari mwaka huu.

Minaj na Remy wamepangiwa kukutana katika tuzo za BET katika kipengele cha ‘Best Female Hip Hop Artist’ ambacho kinawaniwa na wasanii wengine kama Cardi B, Missy Elliott na Young M.A.

Katika vita nyingine ya kumtafuta msanii bora wa Hip Hop kwa upande wa wanaume, Big Sean, Chance The Rapper, Drake, Future, J. Cole na Kendrick Lamar ndio wanawania tuzo hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents