Burudani ya Michezo Live

Nicki Minaj: Nilidhani Mariah Carey ni rafiki yangu kumbe sio

Nicki Minaj alikaa chini na Ryan Seacrest kuzungumza uhusiano wake mgumu na Mariah Carey na tetesi kuwa ataachana na American Idol kama jaji.

http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=ey6CadDO-Bc

Mariah Carey na Nicki Minaj mara nyingi wamekuwa wakizozana mbele ya watazamaji wakati wa show hiyo na kuufanya uhusiano wao kuwa mgumu.

Akiongelea mgongano wake na Mariah, Nicki amesema walianza kama marafiki lakini alikuja kugundua kuwa Mariah hakuwa akijiamini na kumuona kama tishio kwake.

“Imagine mtu ambaye umekuwa ukimpenda katika maisha yako yote …imagine unakutana naye na kisha ghafla unaanza kuhisi kama ulifanya jambo baya kwake lakini hujui ulichokifanya,” alisema Nicki.

“Hivyo ndivyo uhusiano wangu na Mariah ulivyo, na hivyo imekuwa tangu mwanzo. Nilidhani kabisa kuwa sisi ni marafiki, lakini hicho ni kitu kingine nilichojifunza kwamba tasnia hii ni feki sana. unatembea ukidhani kuwa watu ni marafiki zako na kumbe sio.”

“It’s a couple nice hi and byes and then really, you better not step on nobody’s toes. And God forbid you get a little shine. And God forbid you’re maybe witty or quick on your toes or make someone laugh. Then maybe you’re making another person feel insecure. And you shouldn’t have to dim your light to let another person shine.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW