Habari

Nicolas Maduro ashinda uchaguzi kwa kishindo Venezuela

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameshinda tena kiti cha Urais kuiongoza nchi hiyo kwenye uchaguzi uliofanyika Jumapili hii.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huo yaliyotangazwa na rais wa tume ya uchaguzi wa nchi hiyo, Tibisay Lucena, Maduro amepata jumla ya kura milioni 5.8 wakati mpinzani wake Henri Falcon akipata kura milioni 1.8.

Jumla ya kura zote zilizopigwa zilikuwa ni milioni 8.6. Kwa mujibu wa matokeo hayo yanamfanya Maduro kuendelea kuingoza nchi ya Venezuela kwa kipindi cha miaka siata ijayo.

Maduro alianza kuiongoza nchi hiyo March 5, 2013 akichukuwa nafasi ya Hugo Chávez aliyefariki dunia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents