Burudani

Nicole Scherzinger na Lewis Hamilton waachana kwa mara ya nne!

Nicole Scherzinger ameachana na mpenzi wake Lewis Hamilton kwa mara ya nne.

2539A94B00000578-2938882-image-m-102_1423014673639

Muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 36 ameachana na mshindi huyo wa mashindano ya magari ya Formula One, 30, kutokana na uhusiano kuwa wa mbali (Long-distance relationship).

Nicole anadaiwa kuumizwa mno na hatua hiyo. Wawili hao waliokuwa na uhusiano kwa miaka saba wanaachana kwa mara ya nne sasa.

Chanzo kimoja kimeiambia MailOnline: ‘Ulikuwa ni uamuzi wao wote. Umbali uliwatenganisha kwa kipindi kirefu. Wote walikuwa wakitumia muda wao peke yao sababu walikuwa katika nchi mbili tofauti muda wote.

Nicole anaishi Los Angeles wakati Lewis akiishi Monaco.

Tangu waachane, Nicole amekuwa akiliwazwa na familia yake akiwemo mama yake Rosemary na bibi yake ambao husafiri kwenda London (aliko kwa sasa) kumsaidia katika kipindi hiki kigumu kwake.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents