Habari

NIGERIA: Wanafunzi 100 wahofiwa kufa baada ya kuangukiwa na ghorofa, masuala ya ushirikina yahusishwa (+picha)

Zaidi ya wanafunzi 100 mjini Lagos nchini Nigeria wanahofiwa kufariki dunia baada ya kuangukiwa na ghorofa.

Vikosi vya uokoaji vikiendelea na kazi katika eneo la tukio

Ajali hiyo imetokea leo saa 4 asubuhi, hii ni baada ya jengo la ghorofa tatu kuporomoka na kuwafunika wanafunzi hao wa shule ya msingi wilayani Ita Faji.

Mpaka sasa watoto wanne ndio wameripotiwa kupoteza maisha huku juhudi za kuokoa watoto wengine waliofunikwa zikiendelea.

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC, jengo hilo lililobomoka lilikuwa ni Apartments na shule ilikuwa kwenye jengo hilo.

Akizungumza kwenye eneo la tukio, Msemaji wa Jeshi la Uokoaji nchini humo, Ibrahim Farinloye amesema hilo suala geni kwa Nigeria, kila mwaka matukio ya kuanguka kwa maghorofa yanatokea hii ni kutokana na ujenzi uliochini ya kiwango.

Mpaka sasa, Bado hakuna ripoti kamili ya idadi ya watu waliokuwemo kwenye jengo hilo.

Mashuhuda wa tukio hilo, wamesema kabla ya tukio kutokea ulitokea mpepo mkali uliokuwa umeandamana na vumbi na baada ya dakika 10 kupiga kishindo kizito kilisikika cha jengo hilo kubomoka.

Jambo hilo, limezua gumzo na baadhi ya watu wamehusisha tukio hilon na imani za kishirikina.

Mwaka 2016, jengo kubwa la kanisa nchini Nigeria katika mji wa Uyo lilianguka na kuua watu zaidi ya watu 120. Tazama shughuli za uokoaji zikiendelea

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents