Michezo

Nigeria yaungana na timu 11 kuelekea Kombe la Dunia 2018

Timu ya taifa ya Nigeria jana usiku imefuzu kuingia kwenye michuano ya kombe la Dunia baada ya kufanikiwa kuifunga Zambia goli 1-0 kwenye mchezo wa mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2018.

Alex Iwobi mfungaji wa goli pekee la Nigeria.

Nigeria inakuwa ni nchi ya kwanza kufuzu kutoka Afrika na tayari imeungana na nchi 11 zilizofuzu kombe la dunia kutokana mabara mengine.

Ukitoa mwenyeji Urusi nchi nyingine ambazo zimefuzu mpaka sasa niĀ Brazil, Mexico, Ubelgiji, Iran, Japani, Korea Kusini, Saudi Arabia, Ujerumani, Uingereza, Hispania na Nigeria kutoka Afrika.

Nigeria imefuzu kutoka kundi B ambapo kulikuwa na Algeria, Cameroon na Zambia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents