Michezo

Nike imesitisha mkataba na bondia Manny Pacquiao

Kampuni ya vifaa vya michezo ya Nike, imesitisha mkataba na uhusiano na bondia Manny Pacquiao baada ya kuwafananisha wapenzi wa jinsi moja kama wasio na thamani zaidi ya wanyama.

(FILES) In this September 3, 2014 file photo, Filipino boxing star Manny Pacquiao gestures on arrival for a press conference with fellow boxer Chris Algieri in Los Angeles, California. Pacquiao called his boxing showdown with Floyd Mayweather "the fight of my life" as he got down to work pounding the streets and gym in Los Angeles. The eight-division world champion cranked into serious preparations for the May 2 fight after flying in for his training camp from his native Philippines. On March 2, 2015, Pacquiao ran two miles (3.2 km) and shadow-boxed for two rounds, followed by abdominal work and breakfast of steamed rice, scrambled egg, fish and chicken broth. AFP PHOTO / FREDERIC J. BROWN / FILESFREDERIC J. BROWN/AFP/Getty Images

Bingwa huyo wa masumbwi mwenye umri wa miaka 37, ambaye anagombea nafasi ya useneta katika bunge nchini mwake Phillipines, ingawa baadaye aliomba radhi baada ya kuzongwa na dunia kwa kauli yake hiyo.

Kampuni ya NIKE imetoa tamko lake kwa kusema kuwa kauli hiyo ya Manny Pacquiao kama yenye ufinyu wa mawazo.

Manny-Pacquiao-2

Nike inapinga ubaguzi wa ina yoyote ile na kwamba kampuni hiyo imejiwekea historia ya kuwaunga mkono na kutetea misimamo yake dhidi ya haki ya jamii ya wapenzi wa jinsi moja.

Kampuni hiyo ianayojishughulisha na vifaa vya michezo ikaongeza kusema kwamba inavunja uhusiano na mkata na Manny Pacquiao.

Pacquiao aliitoa kauli hiyo wakati akifanyiwa mahojiano kwenye runinga na awali alionekana kutojutia kauli yake hiyo lakini baadaye katika akaunti yake ya Instagram akaitetea kauli hiyo kwa kusema kwamba alikuwa akisema ukweli kwa muujibu wa kilichoandikwa kwenye Biblia takatifu

Baadaye bondia huyo aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba alikuwa haishambulii jamii hiyo ya wapenzi wa jinsi moja,wakati bado alipokuwa akielezea upinzani wake kwa ndoa za mashoga.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents