Burudani

Nikisema tulipane tutavutana mashati – Mzee Yusuph

Aliyekuwa mwanamuziki wa Taarabu, Mzee Yusuph ameeleza kuwa hakutoa amri kwa watu kutosikiliza nyimbo zake kwani yeye hana mamlaka hayo, lakini asingependa kuona jambo hilo likiendelea na wale wanaodai malipo kwa kuwa walinunua muziki wake, yeye kuwalipa ni kitu kisichowezekana.

Mzee Yusuph amesistiza kuwa wanaodai hela na yeye aliwaburudisha pia, na kulipa sauti yake ni vigumu.

“Kwanza sikusema nataka watu wote wasisikilize au iwe amri, laah! mimi sina mamlaka na hakuna mwenye mamla hayo, anayeweza kusimamisha nyimbo zangu dunia nzima ni Allah pekee yake kwa sababu mimi mwenyewe nimeshazipeleka. Halafu mtu mwingine anasema kama ni hela zetu ulizila, umechuka hela zangu, lakini mimi sinilikuburudisha?.

“Haya lipa burudani yangu, maana nikisema tulipane tutavutana mashati, yaani itakuwa tabu, huwezi kulipa sauti yangu,” amekiambia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.

Mzee Yusuph ameongeza kwa kusema, “Mimi nimeulizwa, watu wanataka kuzitumia nyimbo zako, je unawaruhusu?, sasa nikasema kutoa ruhusa siwezi, neno kusema nawaruhusu hilo siwezi na nimeshatoka huko, nikikuambia usizitumie ni shauri yako lakini kusema tumia hilo jambo haliwezekani. Umeamua kuifuta iwe ni juu yako, nitakuomba nisaidie kuifuta mimi naumia ninaposikia, najuta”.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents