Burudani

Nikki Mbishi amdiss Bonta, aisambaza picha ya Joh Makini akiwa guest na msichana

Ile beef kati ya Lunduno (Tamaduni Muzik) la Dar es salaam na Weusi wa Arusha imerejea tena baada ya hivi karibuni Nikki Mbishi kuanza kuwatupia madongo Weusi.

Jana kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mbishi aliisambaza picha ya Joh Makini iliyoleak mtandaoni ambapo rapper huyo anaonekana akiwa kwenye usingizi mzito na msichana kwenye guest.

Katika picha hiyo kuna maneno yasemayo, “Joh Makini wa Mandugu Diggy leta za moto…leta MANUVAAAAAA…mi ni shabiki mkubwa sana wa huyu jamaa…big up kwake aendeleze HARAKATI mpaka madada zetu wakome.” Haijulikani kama ni Nikki ndiye aliyeandika.

Kitendo hicho kimewakera wengi hasa kwakuwa kimefanywa na Nikki Mbishi ambapo watu wanamlaumu kwa kutafuta beef ya lazima na Weusi ambao mara nyingi wamekuwa kimya.

“I can see tamaduni muzik wanaluz direction,m ua fan bt that way is not ryt kwanini ni nyie na weusi tu?acheni utoto let ua talents work instid of beefs zisizo na kichwa wala miguu guys,” aliandika shabiki mmoja.

Wakati huo huo jana kupitia Facebook, Nikki ameudiss wimbo mpya wa Bonta wa kundi la Weusi uitwao ‘Tukutane Maktaba’ kwa kuandika, “Haya sasa twende ki-CONSCIOUS mpaka “TUKUTANE MAKTABA”….#Hahahahaha another WACK SHIT#”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents