Burudani

Nikki Mbishi asimulia alivyokutana na Marehemu Dogo Mfaume

Jana ilikua ni siku ambayo Msanii wa Bongo Fleva, Dogo Mfaume amepumzishwa kwenye makazi yake ya milele. Rapa Nikki Mbishi amelezea jinsi alivyokutana na msanii huyo.

Dogo Mfaume

Kupitia kurasa za mitandao yake ya kijamii, Nikki Mbishi amendika, “Hereni na Kazi ya Dukani ni classic hits za marehemu DogoMfaume. Nilikutana naye Clouds Fm mwaka 2008 akiwa ameitwa na Ruge baada ya kufanya vizuri sana na nyimbo zake.”

Nakumbuka Ruge hakumtambua Dogo Mfaume kwa haraka, nilimsikia Dogo Mfaume akijitambulisha kwa Ruge “Mimi ni Dogo Mfaume, nimepewa taarifa kuwa unahitaji nikuone”. Nakumbuka Ruge alivyostaajabu “Ooh kumbe we ndo Dogo Mfaume, unafanya kazi nzuri sana” ila sikuweza kujua kilichoendelea kwa maana mi nilienda kufuata mpunga wangu wa mshindi wa Freestyle enzi hizo. All in all he was the great entertainer kwenye fani ya uswazi,” Ameandika Nikki Mbishi.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents