Burudani

Nikki Mbishi atoa tahadhari juu ya wimbo I’m Sorry JK ‘atakayeendelea kuusambaza au kuucheza mimi simo’

Msanii wa muziki kutoka Tamaduni Music Nikki Mbishi baada ya kuitwa na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kutokana na wimbo wake I’m Sorry JK, amewataadharisha mashabiki wake kuacha kuusambaza na kuucheza wimbo huo.

Rapper huyo jana alikuwa na kikao na baraza hilo kujadili maudhuri ya wimbo huo, hata hivyo kwa mujibu wa ujumbe wake kwa mashabiki inaonyesha wimbo huo umepiga marufuku.

Alhamisi hii Nikki Mbishi ametoa taarifa hii

Salaam, Baada ya salamu naomba niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na hii ni kwa usalama wao na wangu pia.

Napokea simu nyingi sana zikihitaji maelezo juu ya suala hilo ila kiukweli kwa watakao hitaji taarifa kamili wanaweza kufika ofisi za BASATA,naomba nisiwe msemaji tena juu ya jambo hili.

Tahadhari:
Kwa yeyote atakayeendelea kuusambaza au kuucheza popote pale mimi sitohusika naye maana technology iko huru popote Duniani na siwezi kuzuia watu wasiupate kwa kuwa ushasambaa,hivyo chukua tahadhari ili usijikute mikononi mwa sheria ????????????. #Asanteni sana,naomba msubiri ujio wangu mpya wa #SINGELI na aina nyingine za muziki kama #NAIJA #MCHIRIKU n.k.
MUZIKI NI AJIRA,MUZIKI NI KAZI YANGU.
#Mungu_Simama_Kweli_Idhihirike
Ni wako mtanzania mvumilivu:

Nikki Mbishi @2017

With no offence!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents