Habari

Nikki Mbishi avunja ukimya ‘Sugu sio Mheshimiwa’

Rapa wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Nikki Mbishi amevunja ukimya kwa kumzungumzia Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu kuhusu kesi yake inayomkabili kwa sasa.

Nikki Mbishi na Sugu

 

Nikki Mbishi amesema Sugu sio Mheshimiwa tuu! bali ni kamanada na mpambanaji wa jamii nzima inayomzumguuka.

Mnachoshindwa kujua ni kwamba huyu jamaa kwa sisi wengine sio mwanasiasa tu bali hamasa kwa vijana wasiotaka ndoto zao zifie mitaani,nani alidhani dhana ya Hip Hop uhuni itakufa na mwana Hip Hop kuwa Mheshimiwa hata hivyo Sugu sio Mheshimiwa bali kamanda mpiganaji wa jamii yake yote,“ameandika Nikki Mbishi kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuelezea ushawishi wa kazi zake kwa wasanii wa leo akiwemo yeye.

Tumekua tukisikiliza kazi za Sugu tangu utoto wetu wengine akatuonesha njia kwenye muziki leo anatuonesha njia nyingine na vijana tunahamasika.

Nikki Mbishi anakuwa miongoni mwa marapa wa kwanza kumzungumzia Sugu tangu akumbane na kesi yake ya uchochezi inayomkabili.

Hayo yamejiri ikiwa ni wiki mbili zimepita tangu Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kuwalaumu wasanii wa muziki kuwa wanashindwa kumtetea msanii mwenzao Sugu licha ya kuwa mbele kila kunapotokea tatizo.

Somza zaidi- Jibu la Nikki wa Pili kwa Mhe. Nassari kuhusu Sugu

Sugu na mwenzie Emmanuel Masonga ambaye ni Katibu CHADEMA Kanda ya Nyasa wapo rumande kwa wiki mbili sasa kwa tuhuma za kauli za kichochezi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents