Burudani

Nikki Mbishi kufuata nyayo za Diamond, Vanessa Mdee na Wakazi kwa mwaka 2018 (+video)

Rapa Nikki Mbishi ni moja ya marapa ambao kwa mwaka huu huenda wakafika mbali zaidi kimuziki hii ni kutokana na mapokezi ya kazi zake ikiwemo ngoma yake mpya ya ‘Nimekumiss’.

Habari njema kwa mashabiki wake au wapenzi wa muziki wa Hip Hop ni kwamba mwaka huu, Nikki Mbishi ametangaza kuachia album yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Sam Magoli’ .

Nikki Mbishi amethibitisha hilo kwenye kamera za Bongo5, ambapo amesema kuwa album hiyo itakuwa ni moto wa kuotea mbali hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula.

Akielezea kwanini album hiyo ameeita ‘Sam Magoli’. Nikki amesema mchezaji wa mpira wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta ndiye aliyemvutia zaidi na kumshawishi hadi kuweka jina hilo kwenye album yake.

Kwa ujio wa album hiyo Nikki Mbishi atakuwa ameungana na wasanii wengine kama Diamond Platnumz, Vanessa Mdee na Wakazi ambao kwa mwaka huu tayari wameshafungua pazia la kutoa album.

Hii inakuwa pia ni album ya pili kwa Nikki Mbishi baada ya kuachia ‘Sauti Ya Jogoo’ na ‘Ufunuo’ na ile kanda mseto yake ya Malcom XI.

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents