Nikki Mbishi: Weusi ni watu wasiotaka ‘challenge’ kutoka kwa watu wengine

Hivi karibuni Bongo5 ilikaa kitako na rapper mashuhuri wa kambi ya Tamaduni Muzik kuzungumza machache kuhusu muziki wa Hip Hop nchini pamoja na uhusiano wao na familia ya Weusi ya Arusha inayoundwa na Joh Makini, G-Nako, Lord Eyez, Bonta na Nikki wa Pili.

Katika mazungumzo hayo Nikki Mbishi alisema kuwa Weusi wamekuwa ni tabaka la watu ambao hawataki kuwa na challenge kutoka kwa watu wengine.

“Kwa maana kwamba wao ni NAM, Non Alignment Movement kwa maana kuwa hawafungamani na upande wowote, wao ndio wanaweza, wao ndio wana bendera ya hip hop, wao ndio wana fimbo na mkongojo na ngao ya hip hop wanaongoza mbele kitu ambacho sio kweli,” alisema Mbishi.

“Mimi napenda katika hip hop nikikuchallenge usichukulie beef, fikiria kwanini fulani kanichallenge, kwanini fulani kaniita kwamba wewe ‘wack’ kwanini asimwambie mtu mwingine, jiulize uwack wangu uko wapi? Mimi nikikudiss watu huwaga wanajibiana diss au wanakaa behind the scene, behind the curtain, tunakaa mimi na wewe kwamba, ‘kwani mimi navyorap napungukiwa nini? Mimi nakwamba sikiliza, ‘una mashairi mazuri, una mawazo mazuri lakini sasa unavyowalisha wewe haitakiwi, fanya hivi na hivi.”

Alisema ndio maana Tamaduni Muzik waliamua kuanzisha vilinge ama cypher kwaajili ya kupeana changamoto kama hizo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents