Burudani

Nikki wa Pili akosoa maneno matakatifu ya Mungu juu ya uumbaji wa mwanamke, Kikwete na Billnass wamtolea povu

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nikki wa Pili amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutoa maoni yake tofauti na Biblia juu ya uumbaji wa mwanamke kama vitabu vitakatifu vinavyoeleza.

Nikki wa Pili ametoa maoni hayo kwenye mitandao ya kijamii kwa kusema kuwa sio kweli mwanaume alikuwa wa kwanza kuumbwa na Mungu kama Biblia inavyoeleza, bali mfumo wa zamani ulikuwa mfumo dume na Biblia iliandikwa na wanaume.

Stori inayosema Mungu alimuumba kwanza mwanaume, alafu baadae akaja kumuumba mwanamke kutoka mbavu zake, nadhani iko hivyo kwa sababu imeandikwa na mwanaume na iliandikwa kipindi ambacho jamii zilikua nyuma sana katika haki za kijinsia, ni Stori ya kimfumo dume,“ameandika Nikki wa Pili.

Maoni hayo yalipokelewa tofauti kabisa na mashabiki wake pamoja na wasanii wenzake akiwemo Billnass ambaye alimwambia kuwa amefikia hatua ya  kukosoa Biblia kisa kuoa mwanamke mzuri.

Tumefikia Kukosoa Bible Kweli Nickson ? Inawezekana Mtu Ukipata Mwanamke Mzuri unaweza kusema Chochote,juu ya chochote bila kumhofia yeyote,” ameandika Billnass .

Mwingine aliyejitokeza kumshauri ni Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete ambaye ambaye amemwambia atafakari kwa kina kwani maneno yaliyoandikwa ni matakatifu na ukweli utabaki kuwa hivyo.

Nikuombe umuogope Mungu. Hizo ni hadithi takatifu na ndiyo ukweli. Maana tunakoelekea mtakuja kututhibishia kuwa Tulianza kama nyani na kuwa Evolution is Really. Nadhani hilo ni tatizo. Mengine haya ni ya Mwenyezo Mungu, anataka kutuambia kuwa Mungu anajinsi ya Me,” ametoa ushauri Ridhiwani Kikwete .

Hata hivyo watu wengi waliotoa maoni yao wameoneshwa kukerwa na Nikki wa Pili juu ya mtazamo wake huo.

 

Nikki wa Pili ni moja ya wasanii wa muziki wasomi nchini Tanzania na mara nyingi huwa anaweka mawazo yake kwenye mitandao ya kijamii bila kujali namna mtazamo wake utakavyopokelewa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents