DStv Inogilee!

Nikki wa Pili aungana na Spika Ndugai ishu ya kucha na kope za bandia bungeni ‘mimi napenda urembo wa asilia’

Msanii kutoka kampuni ya Weusi, Nikki wa Pili ameunga mkono kitendo cha Spika wa Bunge, Job Ndugai cha kuwapiga marufuku Wabunge wanawake kuingia Bungeni wakiwa wamebandika kucha na kope za bandia.

Nikki akiwa na mwanadada anayedaiwa kuwa mpenzi wake.

Nikki wa Pili amebainisha hayo alipokuwa anazungumza na kusema amefurahia maamuzi hayo kutokana na yeye kuwa ni miongoni mwa mashabiki wa urembo wa asilia na si urembo wa bidhaa, ambao unafanywa na baadhi ya wadada wa sasa bila ya kufikiria madhara yake hapo baada ye.

“Mimi napenda urembo wa asilia hivyo sipishani sana na Spika Ndugai lakini nafikiri kwa hadhi ya Bunge, Spika ametumia ustaarabu mzuri ambao mimi naungana nao maana walikuwa wanavuka mpaka sana. Watu wanapaswa kuwa makini sana na madhara yatokanayo na vitu bandia, kiukweli mwili wa binadamu umegeuzwa kuwa bidhaa kwa sasa”, amesema Nikki wa Pili.

Pamoja na hayo, Nikki wa Pili ameendelea kwa kusema kuwa “sasa hivi tupo katika kipindi mwili wa binadamu umegeuzwa kuwa bidhaa, na ndio maana unakuta kuna nywele bandia, kucha, kope, maziwa bandia pamoja na kubadilisha ngozi rangi”.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW