Burudani

Niko tayari kufanya kazi tena na Said Fella endapo atanitafuta tuongee – Juma Nature

Juma Nature amesema yupo tayari kufanya kazi tena na meneja wake wa zamani Said Fella, endapo Fella atamtafuta ili wazungumzie.

Nature

Kauli hiyo ya Nature imekuja baada ya Fella kutangaza kuwa anampango wa kufanya kazi na Nature baada ya miaka mingi kupita toka Nature ajiondoe TMK Wanaume Family na kuanzisha kundi lake la Wanaume Halisi.

“Idea yake ni nzuri kibinadamu, anatakiwa akae na mimi nijue lengo lake kwanza ni nini yeye ni binadamu kama mimi,” Nature ameimbia 255 ya Clouds Fm.

“Mi sijaongea na Fella siwezi kukudanganya, lakini kama Fella atakuja akiona anataka tufanye kitu kizuri na yeye ajijenge kwasababu hapa mimi naimani kabisa mimi ni nguzo kwa sanaa ya bongo ni nguzo sana, sasa yeye kitu kama hicho kaishakifahamu anatakiwa yeye anitafute mimi tukae chini bwana kuna hili na hili. Yeye kwasababu kaongea yeye mi sikuongelea kitu, na sitaki kulifatailia sana swala hili mpaka yeye mwenyewe atakaponitafuta mimi, kwasababu Nature ana watu, Nature hana mtu mmoja.”

Said Fella amesema kuwa yuko tayari kumtafuta Nature ili wazungumze na kufanya kazi tena.

“Kweli nitamtafuta kwasababu mwanangu, la msingi kwanza mi mwenyewe ndo niko busy busy […] mwenyezi Mungu akijalia nikipata nafasi ntaenda kumwambia mwanangu eeh tuendelee na kazi, ukweli sijaongea naye lakini sisi binadamu na hii dunia […] Kwa hiyo mengine yote yapite tujenge nchi na mwanangu ndo hilo la msingi.” Alisema Fella.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents