Burudani

Niler Bernard afunguka wanavyobaguliwa na kutoswa dili za matangazo nchini SA (Video)

Mwanamitindo Niler Bernard ambaye pia aliwahi kuwa mshindi wa Tanzania Top Model 2013, amefunguka jinsi wanavyobaguliwa nchini Afrika Kusini na wanavyonyimwa dili kubwa za kufanya matangazo kutokana na rangi zao.

Akiongea na Bongo5,Mrembo huyo mwenye mika 20, ambaye anafanya kazi katika kampuni ya uanamitindo ya Boss Models iliyopo nchini humo, amesema wanamitindo wenye rangi nyeupe [wazungu] ndio wanaopewa nafasi kubwa katika kupewa dili hizo wakifuatiwa na wanamitindo wengine ambao wamechanganya rangi.

“Ukifika South Africa unaona kabisa kuna tabaka la wazungu, weusi na kuna wengine waliochanganyika kati ya weusi na wazungu. Kwa mfano ikitokea kazi wamerequest black models, wana-request a dark skin black model, na a lot of commercials kwa sababu ziko very international wanakuwa wanachagua white models. Na wakichagua black models wanachukuwa wale ambao if either a dark skin na kama na kama haupo dark skin na haupo mixed that means wewe your standing alone,” amesema Niler.

“Watu weiupe ndio wanapata a lot of gigs, watu weusi ni mmoja, watatu. Hata Commercials ukiangalia unakuta labda tangazo la watu 20 unakuta watu weusi wawili au watatu ndio wapo,” ameongeza.

“Nilienda kabisa tena wanatafuta mtanzania, I was telling my friend, am getting this one. Unajua kabisa this is foem home, siwezi kulikosa. Mimi nilikuwa najua wanataka a Tanzanian looking girl, I don’t need to be a Tanzanian looking kwa sababu mimi ni mtanznia, so obviously mimi ni mtanzania. Nikaenda pale na all the confidence but I never booking the job, and that really broke my hert.”

Niler amesema tangazo hilo alilotoswa lilikuwa la DSTV na lilikuwa linathamani ya zaidi ya Rand 30,000 ambapo kwa fedha za kitanzania ni zaidi ya shilingi milioni sita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents