Michezo

Niliingiwa na nywele machoni licha ya kuingia nusu fainali – Rafael Nadal

Mchezaji tenis namba moja katika viwango vya ubora duniani, Rafael Nadal ametinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya China ‘China Open’ baada ya kumfunga John Isner.

Nadal amemshinda John Isner kwa jumla ya seti 6-4 7-6 huku akipata tatizo katika macho yake.

Baada ya ushindi huo Nadal amesema “Kunakitu kimekuja machoni mwangu,” amesema Nadal ambaye anafukuzia ubingwa wake wa sita kwa mwaka huu.

Nadal ameongeza “Nafikiri ilikuwa kama nywele hivi kutoka katika mpira ama kitu fulani kimeingia machoni mwangu na kunisumbua.”

Nadal sasa atacheza na Grigor Dimitrov katika michuano hiyo ya wazi ya China katika hatua ya nusu fainali huku Krygios nae akitinga hatua hiyo kwa ushindi wa seti 6-0 3-0 dhidi ya Steve Darcis na sasa atacheza na Alexander Zverev hatua inayofuata.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents