Aisee DSTV!

“Nilijilipia mahari mwenyewe ili niolewe, Wanaume wanaumiza sana” – Mchekeshaji Anne Kansiime

Mchekeshaji maarufu nchini Uganda, Anne Kansiime amefunguka kwa mara ya kwanza namna alivyonyanyaswa na kuumizwa na aliyekuwa mume wake, Gerald Ojok .

Kansiime amesema wakati wakiwa kwenye mahusiano, Yeye ndiye alikuwa anatoa kila kitu na hata kipindi cha kuolewa alimpatia mumewe huyo fedha ya mahari ili akatoe kwa wazazi wake.

Watu wengi wanandhani mimi nimechanganyikiwa hapana, Mapenzi yaliniumiza kipindi tulivyoachana na mwenzangu ila kwa sasa nipo na furaha ya kutosha. Siwezi tena kuumia kwa mtu ambaye nilikuwa najihudumia mwenyewe na hata mahari nilijilipia mwenyewe ili anioe. Nadhani kila mtu anahistoria yake kwenye mahusiano sikutaka kuongea hadharani lakini ukweli ni kwamba wanaume wanaumiza sana.“ameongea Kansiime katika video aliyoiweka kwenye akaunti yake ya mtandao wa YouTube ya Kansiime Anne.

“Mwanamke ili uonekane umeolewa ni lazima mumeo awe karibu na wewe kila mahali, Kanisani mnaenda pamoja mkiwa mmeshikana mikono, Akuhudumie , Akulipie mahari lakini hayo yote hayajawahi kufanyika kwenye mahusiano yetu,”

Kansiime na mumewe waliachana mwaka 2017 na hajawahi kueleza sababu za msingi za kuachana na muwewe huyo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW