Burudani

Nilijua tangu mwaka 2012 kuwa Kanye West atakuja kugombea urais – Big Sean

Wengi walishangazwa na tangazo la Kanye West hivi karibuni kuwa atagombea urais wa Marekani mwaka 2020 lakini Big Sean anasema aliliona hilo mapema.

Big-Sean-Kanye-West-Bendxl

Rapper huyo aliyetumbuiza kwenye iHeartRadio Music Festival Jumamosi iliyopita, Sept. 19, aliuambia mtandao wa Billboard kuwa alitabiria uamuzi wa Kanye kuwania urais miaka kadhaa nyuma.

“Nililiona hilo kama mwaka 2012, kuwa Kanye atakuja kugombea urais. Ana mawazo mengi sana. Anapenda anachofanya,” alisema. “Nje ya hapo lakini najua ni mtu tofauti, yeye ndiye alinigundua mimi.”

“Mtu yeyote anayeweza kumsikiliza mtoto akirap kwenye kituo cha redio na na kuona kipawa chake na kukifuata, unajua ni mmoja wa watu wakubwa kuwahi kutokea,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents