BurudaniUncategorized

Nilikuwa namuelekeza mdogo wangu Dogo Janja – Nedy Music

Msanii wa Bongo Flava chini ya label ya PKP, Nedy Music amesema si kweli kuwa haelewani na Dogo Janja bali alikuwa anamuelekeza baadhi ya mambo.

Miezi miwili iliyopita Nedy Music aliiambia Bongo5, “nachoweza kusema ni kwamba Dogo Janja asaidiwe, ana zeeka vibaya kila siku anabadilika, uwezo wake wakufikiri unapungua kila siku”. Kauli hiyo ilikuja baada ya Dogo Janja kutamba yeye ndiye msanii anayeongoza kwa kuvaa vizuri Bongo.

Sasa leo hii Nendy Music akizungumza na Daladala Beats ya Magic Fm amesema alikuwa akimuelekeza Dogo Janja kama mdogo wake na sasa ameanza kuelewa.

“Dogo janja tunaongea tena ni washikaji kabisa, ni vitu vidogo nilikuwa namuelekeza mdogo wangu na si vibaya akawa ananisikiliza na hatimaye ananisikiliza naona kidogo kidogo anapanda,” amesema Nedy Music.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents