Soka saa 24!

Nilimpigia simu S2kizzy baada ya kusikia amezawadiwa gari na Rayvanny – Mr T Touchez

Watayarishaji wa muziki hapa nchini wamekuwa wakilalamika kutopata wanachostahili kutoka kwenye kazi za muziki wanazo zitengeneza na badala yake wasanii ndio wanaonufaika zaidi, kwa hivi sasa hali imeanza kubadilika kutokana na watayarishaji kuanza kuona mafamanikio kufuatia malipo wanayoyapata kutoka kwa wasanii hao.

Hivi karibuni mtayarishaji S2kizzy alipewa zawadi ya gari kwenye siku yake ya kuzaliwa na msanii wa WCB, Rayvanny ikiwa ni sehemu ya shukrani baada ya kumtengenezea nyimbo kadhaa zilizovuma ikiwemo ‘Tetema’ aliyofanya na Diamond Platnumz

Kufuatia tukio hilo Mtayarishaji mwingine, Mr T Touchez amesema alichokifanya Rayvanny ni funzo kubwa kwa wasanii wengine waliopo kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya katika kuhakikisha wanathamini mchango wa watayarishaji (Producers)

‘’ nilimpigia Rayvanny nikamwambia umeonesha utofauti na utawafunza wasanii wengi kwamba hii kitu inatakiwa mwisho wa siku iwe hivi, kwasababu hawa watu hawapati kitu na kama huwezi kujiongeza huwezi kufanya show huwezi kufanya kitu kingine mwisho wa siku unajikuta umeshatengeneza hit lakini huwezi kupata unachoitaji kwenye maisha’’ Touchez amwambia Lil Ommy na AmmyGal kwenye kipindi cha The Playlist.

Aidha, T amesema alizungumza pia na S2kizzy kumpa hongera kutokana na zawadi aliyoipata ambapo alikiri kutokutegemea kupewa zawadi hiyo.
‘’S2kizzy nimechati nae akanambia mimi mwenyewe sijategemea kaka yani nimekutana nayo tu, huyo jamaa ntampa mabiti kibao’’ ameongeza T-Touchez

Source: Times FM

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW