Burudani

Niliogopa umati wa watu nikakimbia – Mo Music

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Mo Music amesema hawezi kusahau alivyolikimbia jukwaa la Fiesta jijini Mwanza mwaka 2014.

Kwa mujibu wa msanii huyo ameeleza kuwa alishuka katika jukwaa hilo baada ya kuona umati mkubwa wa mashabiki waliojitokeza katika uwanja wa CCM Kirumba.

“Fiesta ya mwaka 2014 mkoani Mwanza nilijikuta nikilikimbia jukwaa kutokana na umati mkubwa wa mashabiki waliokuwepo kwenye uwanja wa CCM Kirumba, ile nachungulia nilikutana na watu zaidi ya elfu 20. Nilishtuka nikakimbia nyuma ya jukwaa, baada ya kuzoea mazingira nikarudi tena jukwaani kufanya show,” Mo ameliambia gazeti la Mtanzania

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents