Michezo

Nilipanda ulingoni nikiwa na msiba wa baba yangu – Campbell

Bondia muingereza, Luke Campbell ametoa ya moyoni juu ya taarifa ya kifo cha baba yake mzazi mzee, Bernard ambaye alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa kansa akiwa amefikisha umri wa miaka 58.

Campbell ameeleza kuwa alipata taarifa ya kifo cha baba yake wakati alipokuwa anajiandaa kupambana na Jorge Linares pambano la ubingwa wa WBA na kusema kuwa aliamua kuendelea na maandalizi ya pambano mpaka alipoingia ulingoni hakutaka mtu yeyote kufahamu kilichomkuta.

“Laiti kama kungekuwa na mtu amegundua ukweli juu ya hali yangu kwa wakati huo nisingemkubalia ningekataa maana nisingependa kambi ya mpinzani wangu itambue udhaifu niliyokuwa nao”. Campbell alikiambia chombo cha Habari cha BBC Sport.

Campbell mwenye umri wa miaka 29 alishinda katika mchezo huo kwa pointi amesema

“Kitu pekee kilichonipa ujasiri wa kuendelea na mpambano ilikuwa ni kwa sababu nilikuwa nafahamu baba angu alikuwa anahitaji mimi nipambane siku zote na kuhakikisha nashinda”.

“Pengine nililia mara moja kwa siku na kuzuiya hisia zangu na baada ya pambano ndipo nikalia zaidi”.

Campbell aneongeza ” Nilipata habari nyingi sana baada ya wiki mbili kupita, watu walikuwa wakiniandika vibaya juu ya msiba wa baba yangu nikaamua kuwa kimya na niliwafunga vinywa vyao kwakuwa nilishinda na kufanya kile ambacho baba alikuwa anatamani”.

Bingwa huyo wa medali ya dhahabu ya London uzito wa Lightweight Jumamosi usiku amepigwa kwa pointi katika mchezo wa masumbwi dhidi ya bingwa wa Venezuela.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents