Nilipoitembelea Zanzibar

Zanzibar_round_about_face
BAADA ya ukongwe wa barabara nyingi za Zanzibar sasa mabadiliko yaanza kujitokeza kwa baadhi ya barabara kwa kurekebishwa na kuziweka katika hali ya kisasa zaidi. Nimezunguka karibia sehemu kubwa ya mji huo, nikagundua baadhi ya barabra za kutoka na kuingia mjini zipo kwenye matengenezo, ingawa sikujua ni ya umbali wa kilomita ngapi.

 

 

Moja ya sehemu ambayo nimeikuta ikitifuliwa na kutengenezwa upya na njia panda ‘Round about’ ya Amaan, ambayo inatokea mjini, kwende Sokoni Mwanakwerekwe, Shamba na Daraja bovu.
Zanzibar_Soko_kuu
Pia Barabara ya njia panda ya kuelekea mjini Darajani, Chuo Kikuu, Mwanakwereke (Soko Kuu) na kurudi uwanja mkuuwa Amaan, nao nimeukuta imewekwa vizuizi, yaani ikimaanisha ujenzi unataka kuanza.

Zanzibar_barabara_Tumbatu
Ila kuna barabara kama ya kutokea Posta Kariakoo (Ya Zanzibar) kuelekea viwanja vya kufanyia mikutano vya Mtumbapu, na kupitiua kwenye wizara nyingi hadi Uwanja wa ndege wa Aman Abed  Karume,  nimeikuta ipo katika hali hii,  ila naamini nazo zipo kwenye mikakati kama sio leo basi siku yoyote.

Zanzibar_magari_ya_mawe
Pembezoni mwa barabara moja ambayo ipo kwenye mikakati ya kujengwa nilikutana na magari kama matano ama saba hivi, yenye mawe makubwa, nikadadadisi kwa kuuliza je Mawe haya nayo yapo kwenye huo ujenzi wa barabara. lakini kuna mtu mmoja akanijibu kwamba haya ni kwaajili ya ujenzi wa makazi ‘Nyumba’ ya watu, ambazo wanasema bila ya kuweka msingi wa mawe kama hayo utakuta nyumba inamong’onyoka na kudondoka. lakini mtu mwingine akanijibu kwamba hayo yapo katika mradi huo wa ujenzi.
Zanzibar_barabra_ya_Aman
Nikakutana na  barabara hii ambayo ni muhimu, maana ndiyo inayoingia mjini moja kwa moja na inatoka hadi  kuelekea kwenye uwanja wa Taifa wa Amaan, nayo nimeikuta hivi.
Zanzibar_Punda
Zaidi ya barabara hizi na usafiri wa gari, pikipiki, baiskeri lakini pia nikakutana na usafiri wa Ng’ombe na Punda. Ila sijajua kama kweli kuna haki za wanjama katika maeneo fulani, maana nilikuta punda anamzigo mzito ila anakula bakora za nguvu ili kwenda lakini aligoma.

Nilihisi atakuwa amechoka na mzigo mzito kwakuwa kipindi hicho jua lilikuwa kali sana, ila roho iliniuma pale ilipochuliwa bonge la gongo la mti na kupigwa nalo na ndipo akaanza kutembea na safari ikakolea, na hapo ndipo nikaamini kweli….PUNDA AFE LAKINI MZIGO WA BWANA UFIKE.
Zanzibar_Kariakoo
Nikaona haitoshi nikatembelea mpaka Viwanja vya watoto wanavyotembelea siku za sherehe za sikuku, ambavyo nilipenda hata mimi kuingia kuchezea japo kidogo, kutokana na kuviona kwa juu nikamuuliza mwanafunzi mmoja juu ya michezo ya hapo, ndipo akanijibu kwamba  vitu vingi vilivyokuwa humo ndani havifanyi kazi tena. Nilipouliuza kwa nini, niliambiwa havina uangalizi mzuri jambo linalopelekea kufaa kifaa kimoja kimoja, ingawa fedha zinapatikana  wakati wa sikukuu. Kweli nilipozunguka kwenye ukuta nilikutana na hali kama hii, yaani hata njia ya vigari vya michezo  nilikuta imekufa kabisa, na hata baadhi ya michezo nikagundua haitaweza kufanyika tena kutokana na vifaa vyake na njia za michezo hiyo  kuwa kukuu na kuharibika kabisa.
Zanzibar_Kijijini

Nikaona nisiishie mjini, nikatembee Shamba (Kijijini), na huko nikakutana na nyumba nzuri za vijinjini ambazo hata mimi huwa nazipenda, ila nikagundua msitu wao ni mazao. Yaani msitu umepamba kwa miembe, mishokishoki, minazi,michungwa, mti wa mdalasini, karafuu, zaituni, migomba na kila aina ya miti ya mazao na viungo ambavyo vinaunda msitu huo wa kuvutia.

Zanzibar_Magogo
Sikuwa na shaka ya kuingia ndani ya msitu kidogo kwakuwa Wazazibar ni wakarim, lakini nilipofika ndani ya msitu nikagundua jambo lingine. yaani miti hiyo hiyo hususani ya Minazi na Miembe, ikikatwa kwa wingi kwaajili ya kuchoma mkaa na kuni za kupikia hapo kijijini na zingine huletwa mjini kwaajili ya matumizi kama hayo, pia miti mingine ikikatwa kwa wingi kwa matumizi ya ujenzi wa nyumba za mjini na kijijini.

Zanzibar_Matunda
Nikaamini kama wataendelea na harakati hizo watakuwa na miaka michache ya  kumaliza miti hiyo ya matunda, na haya matunda ninayokutana nayo njiani hayatakuwepo kwa wingi kama ninavyoyaona hivi sasa. Nikajua siku inakuja kama hawataweja kuzuia jambo hili mapema ama kuweka mpangilio maalum, wa ukataji hiyo miti matatizo mengi yatatokea hasa haya yanayotokana na mabadiliko ya hali nchi.

Na hapo ikawa ndiyo safari yangu imekwisha ya kurudi mjini na kuendelea na tamasha la Filamu Zanzibar, ZIFF

By Mo One’s

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents