Michezo

Nilitamani kucheza kama Steven Gerrard Enzi za Utoto-Keita

Nilitamani kucheza kama Steven Gerrard Enzi za Utoto-Keita

Kiungo mpya wa majogoo wa Anfield Liverpool Naby Keita amefunguka na kusema kuwa alitamani sana kucheza kama kiungo wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard enzi za utoto wake wakati akicheza mpira mtaani nchini kwao Guinea.

kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 aliyesajiliwa kutoka katika klabu ya RB Leipzig ya nchini Ujerumani kwa uhamisho wa ada ya Euro mil 57,tayari amekabidhiwa jezi yeye namba 8 mgongoni ambayo alikuwa akiivaa mkongwe huyo ambaye kwa sasa ni kocha katika klabu ya  Rangers.

akiongea na kituo cha Espn Keita amesema “Baba yangu alizungumza na mimi nilipojiunga na Liverpool na amenieleza jinsi gani anavyoipenda Liverpool hata sisi wakati tunacheza mpira mtaani tulikuwa tukivaa Jezi za Liverpool.”

Keita ameongeza “Kwa sababu mimi ni kiungo na Gerrard pia alikuwa kiongozi katika upande huu, haiwezi kuwa mtu mwingine yeyote isipokuwa Steven Gerrard ambaye ningependa kwa wakati huu wote ninapokuwa nacheza, nataka kuwa kama yeye”

keita amemaliza kuwa kamwe hataiangusha hadhi ya Jezi namba 8 na anataka kuvaa viatu vya Gerrard ipasavyo.na alishtushwa sana na maneno ya Gerrard aliposema kuwa “Kila mtu yuko hapa kukusaidia ili uweze kuiendeleza namba 8.”huku akimaliza kuwa “Ninajua ni namba kubwa hapa na ninafurahi sana kuivaa lakini pia ni kitu ambacho sitakiwekea shinikizo lolote zaidi.”

Liverpool wamefanikiwa kufanya usajili mzuri katika maeneo tofauti tofauti kwa lengo la kukisuka kikosi baadhi ya sajili ambazo wamezifanya ni pamoja na kuwasajili ( Naby Keita – kutoka Leipzig, £52.75m, Fabinho – kutoka Monaco, £43.7m, Xherdan Shaqiri -kutoka  Stoke, £13.5m, Alisson Becker – kutoka Roma, £67m na  Isaac Christie-Davies – kutoka Chelsea, bure.

 

By Ally Jei.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents