Habari

Nilitamani kusoma chuo kikuu lakini… – Eric Shigongo

Mjasiriamali na Mtunzi wa vitabu mashuhuri nchini Tanzania, Erick James Shigongo anatarajia kurudi shule na kusoma elimu ya shahada baada ya kuhangaika muda mrefu kutafuta nafasi hiyo, huku akisukumwa na masimango na matusi ya mitandaoni.

Eric Shigongo

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Erick Shigongo ameandika waraka mrefu akielezea safari yake kitaaluma na furaha aliyonayo, ya kuweza kufikia ndoto yake ya kuwa na elimu ya chuo kikuu, licha ya kuwa na mafanikio makubwa kwenye kazi zake za utunzi na maisha kiujumla.


“Ndoto imetimia, hatimaye naingia Chuo Kikuu, nikiwa mtoto nilitamani sana kusoma hadi chuo kikuu lakini sababu ya umasikini na mazingira magumu hasa shule nilizosoma, sikufaulu mtihani wa darasa la saba, nikarudia darasa la saba katika shule nyingine lakini bado sikufaulu, nilijiona mjinga! Nikajaribu kupitia njia ya ‘vikozi’ vidogo ili hatimaye niingie chuo kikuu lakini sikufanikiwa, nikaachana na ndoto hiyo na kuanza ujasiriamali”
, ameandika Erick Shigongo.

Erick Shigongo alendelea kuandika akisema kuwa ndoto yake hiyo imefanikiwa baada ya kujiunga na mfumo wa RPL ambao hufanya watu wenye uzoefu fulani katika jamii bila kuwa na elimu, na kuwapa nafasi ya kusoma elimu ya juu, ndipo alifanikiwa kupata nafasi mwaka huu, baada ya kufeli mwaka jana.

“Nikakusanya vitabu vyangu ambavyo nimekwishaandika na kuvipeleke Tume ya Vyuo Vikuu na kuomba niruhusiwe kufanya mtihani huo, nikaruhusiwa, mwaka jana nikafanya na kufeli, sikukata tamaa, mwaka huu nikafanya tena na kufaulu, hivyo mwezi wa tisa ninaanza mwaka wa kwanza “, ameandika Erick Shigongo.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents