Nilitamani sana nimwambie Nikki wa Pili aache muziki – Joh Makini

Leo ni siku ya kuzaliwa ya rapa kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili ambapo mashabiki pamoja na ndugu zake wa karibu wametumia mitandao ya kijamii kumtakia heri na baraka katika maisha yake.

Joh Makini ambaye ni kaka wa rapa huyo akiwa katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, amefunguka namna alivyotamani kumkataza mdogo wake huyo kufanya muziki kutoka na changamoto ambazo alikutana nazo.

“Nilikuwa naambiwa na watu kuwa mdogo wangu 9Nikki wa Pili) anachana na sikuzingatia na hata wakati anarekodi GoodBoy sikuwepo, kuna kipindi nilikuwa natamani nimwambie asifanye muziki kutokana na changamoto na mazingira ambayo tulikuwa tunapitia ila nilikuwa nashindwa sababu alikuwa ananiprove wrong kwenye kazi zake,” alisema Joh Makini.

Mapema ya leo hii Nikki alianza kusherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kwenda kutoa msaada wa vifaa vya kujifunzia katika shule za msingi.

“Asubuhi nilienda shule kupeleka vitabu na mapokezi ya shule yalikuwa makubwa kwani nilienda toka wiki iliyopita kuomba nafasi na walikubali na leo ikiwa ni siku ya kumbukizi yangu ya kuzaliwa nikaona niende kupelea vitabu,” alisema Nikki.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW