Nilivaa hadi kigodoro – Dogo Janja katika video yake Mpya

Wakati mjadala ukiendelea kuhusu video mpya ya Dogo Janja ‘Wayu Wayu’, msanii huyo ameikingia kifua video hiyo baada ya kutokea na muonekano wa kike.

Hitmaker huyo wa ngoma ‘Ngarenaro’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio alichofanya katika video hiyo ni ubunifu na baada ya hapo maisha yake yanandelea kama kawaida na si vinginevyo.

“Nilivaa hadi kigoro, mwisho wa siku unafanya kitu lakini heshima yako itabaki pale pale sio unaigiza hivyo halafu unaendelea kuwa na miyeyusho ya aina hiyo hapo itakuwa sivyo, umeigiza umemaliza umerudi umekuwa mwanaume,” amesema.

Video ya Dogo Janja ambayo imeongozwa na Nisher ilitoka March 9 mwaka huu na hadi sasa ina views zaidi ya 300,000 katika mtandao wa YouTube ikiwa namba moja katika trend.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW