Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Nimeachana na Nay kisa ana wanawake wengi – Nini

Aliyekuwa mchumba mpya wa Nay wa Mitego, Nini amedai ameachana na rapa huyo kwa madai ana wanawake wengi.

Muimbaji huyo alithibitisha kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM kwamba ni kweli alikuwa anatoka kimapenzi na rapa huyo ambaye alishirikiana naye kwenye wimbo, ‘Niwe Dawa’.

“Nay ana wanawake wengi sana, nimevumilia nikaona basi kila mtu achukue hamsini zake,” Nini aliuambia mtandao wa Samisago “Nimeshamsikiliza zaidi ya mara mbili lakini naona habadiliki nikaona bora kukaa pembeni,”

Muimbaji huyo amedai kuachana kwake na rapa huyo sio mwisho wa muziki wake kwani anajipanga upya na kuja kivingine.

Nay bado hajazungumza chochote kuhusiana na ishu hizo kwani kili akitafutwa kupitia simu yake ya mkononi hapatikani.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW