Burudani

Nimefanya kolabo karibia 600 – Mr Blue

Msanii muziki wa Bongo Flava, Mr Blue amesema amefanya kolabo takribani 600.

Kauli ya msanii huyo inakuja mara baada ya kuwepo taarifa kuwa kuna baadhi ya mistari yake imekuwa inajirudia kwenye baadhi ya ngoma anazoshirikishwa hasa na wasanii underground. Akizungumza na E-Newz ya EATV amesema hilo linaweza kutokea kutokana na wingi wa kazi anazofanya.

“Juzi tulikuwa tunahesabu na watu nimefanya kolabo karibia na 600 na washikaji tangia nimeanza game,” amesema Mr Blue.

“Kwa hiyo kurudia sometime inaweza ikatokea kwa sababu sijui niliimba kwa nani na nani, kwa hiyo inatokea kama binadamu” ameongeza.

Mr Blue ni miongoni mwa wasanii waliofanya kolabo nyingi zaidi kwa hapa Bongo, ameshafanya na wasanii wakubwa kama Lady Jaydee, Diamond, Alikiba na wengineo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents