Burudani

Nimeirudisha heshima ya Bongo Movie kama enzi za Kanumba – Wema Sepetu

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Mrembo Wema Sepetu ambaye yupo nchini Rwanda tangu Jumatano ya wiki hii, amesema ndiye aliyeifufua tasnia ya Bongo Movie iliyokufa baada ya kifo cha Kanumba.

Wema Sepetu katikati.

Wema amesema marehemu Kanumba alipofariki  hata kiwanda cha Bongo Movie kilionekana kuyumba kwani alikuwa ndiye nguzo muhimu kwenye ramani ya filamu Tanzania.

Zamani Bongo Movie ilikuwa inafanya vizuri sana enzi za marehemu Steven Kanumba, alivyofariki kama na yenyewe ikafa. Tumekuwa tukiomboleza kifo chake na kifo chake kimetusababishia mazingira mabaya sisi kama waigizaji  kwa sababu tuko kwenye fani moja. Wengi wetu tumejikuta watu wanaona Bongo Movie haina mashiko.“amesema Wema Sepetu kwenye mkutano na Waandishi wa Habari jijini Kigali nchini Rwanda na kuelezea jinsi alivyoinyanyua Bongo Movie baada ya kifo cha Kanumba.

Kwa bahati nzuri mimi nimeweza kuirudisha tena Bongo Movie back to where it was (ilipokuwa enzi za Kanumba) baada ya kutoa filamu yangu ya Heaven Sent. Bongo Movie kama Bongo Movie zilikuwa zimelala kiukweli kabisa mpaka nilipozindua filamu yangu hiyo na nimeweza kuiweka kwenye application yangu kumekuwa kuna muhemko, yaani waigizaji wengi hata mkiwaona kwenye mitandao ya kijamii wanashoot, wanafanya vipindi, yaani Bongo Movie haijafa ni kazi nzuri tu tumeshindwa kuziweka sokoni. Tukiwa tuna kazi nzuri tukafanya vitu ambavyo vitapendwa na watu Bongo Movie itakuwa imara tena Inshallah!“.

Steven Charles Kanumba almaarufu The Great alifariki katika mazingira ya kutatanisha mnamo mwezi Aprili 2012 akiwa chumbani kwake na mpenzi wake Elisabeth Michael ‘Lulu’ ambaye mwezi huu amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumuua Kanumba bila kukusudia.

Soma zaidi – Muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ atupwa jela miaka miwili

Msikilize hapa Wema Sepetu akizungumza na Waandishi wa Habari nchini Rwanda ambako alienda kwenye  tamasha la KFM Instagram Party ambalo limefanyika jana ijumaa. (Video by habaripevu.com)

https://youtu.be/Jdzy9tCNPSk

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents