Burudani

Nimejisikia kuwatania kidogo AY, Fid Q, Roma na Izzo Bizness

Rafiki yangu Boaziz Samson amewahi kuniambia “neno na jambo lolote ni utani na unaweza ukamwambia mtu neno lolote lile na akaona ni utani isipokuwa inategemeana na wakati unaotania na mtu unayemtania utani huo.” Basi mimni leo nimeamua kutania huku nikiamini nimezingatia ushauri wa rafiki yangu Boaziz, japo ninaowatania hata hawanifahamu.

Umemuona Fid Q wa sasa? Siku hizi anatoa video kali huku akiwa na warembo pembeni wakidance naye! Fid q huyu huyu ambaye mtaani anajulikana kama bandidu leo amefanya watu waone kweli inawezekana. Moyoni yeye ni hardcore usoni tumuone tu bishoo. Kweli nyakati zinaenda kwa kasi sana,actually nimesema natania don’t take it seriously bro.

Halafu vipi umemsikia Roma yule mwanaharakati wa Mr President,Tanzania na Viva Roma Viva,leo ameachana kabisa na zile mambo siku hizi yeye yupo na K! Heeh? Kunanii ndugu yetu au unaogopa kuimba zile mambo zetu kisa unaogopa sebene la uncle Maguu? Siamini uoga umeanza lini bhanaaa….Hopefully Roma unakumbuka nimesema natania bro!

Hii nyingine noma kabisa,unamfahamu Izzo Bizness,mnyamwezi wa ukweli kabisa wengine hupenda kumwita Jay z wa mbeya,siku hizi yupo na mtoto mmoja mkali anaitwa Abela, anahit na goma lao Umeniweza eti niamini Izzo B kamuacha yule mtoto na wanafanya kazi tu? wapi wewe Bwana Emanuel tangu lini Simba akamuona suala aliyenona akikatiza mbele yake halafu akamuacha hivi hivi? Hhahaha am just joking home boy ila kiukweli siamini!

Ukitaka kuamini hakuna mkate mgumu mbele ya chai basi ona hii hapa! Yeye hujiita Zee na wote tunajua AY ni moja ya watu wasiopenda mambo yao binafsi kujulikana hadharani ila juzi kati hapa bwana ambwene amefichua siri aliyoificha kwa miaka nane!? Kwamba tu uliamua mwenyewe kaka hahah hakuna wewe utakua ulichimbwa biti! Kama huweki open this time, it’s over between me and you.’ I am just joking bro ila miaka nane umeficha man?

By: Eliezer Gibson ”greencity native”

Instagram:gibson_elly

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents