Nimekuwa nikifuatilia mazoezi ya AJ kwa sasa nipo tayari – Parker

Mpinzani wa Anthony Joshua ambaye anatarajia kukutana naye mwezi ujao bondia, Joseph Parker amekiri kufuatilia mazoezi ya maandilizi ya Joshua katika kuelekea pambano lao Machi 31 mwaka huu.

Hayo yamekuja katika kipindi hiki ambacho Joshua amerejea katika kituo chake cha mazoezi huko Sheffield English Institute of Sport na kutupia picha ikionyesha namna mwili wake ulivyojengeka.

Parke alivyo ulizwa namna anavyo yaona mazoezi ya Joshua amesema “Ukimtazama na kuyaangalia mazoezi yake anayofanya ni kama anafanya vitu vipya na kuonekana kumuwia ugumu na kuonyesha kuwa anajiandaa kufikisha raundi 12, amesema Joseph Parker kupitia mahojiano yake na Sky Sport.

Pambano la Joseph Parker raia wa New Zealander  dhidi ya Muingereza Anthony Joshua linatarajiwa kufanyika  Las Vegas  katika uwanja wa Cardiff  Machi  31 mwaka huu.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW