Habari

Nimemfahamu Rais Magufuli kabla hajawa Rais – Humphrey Polepole

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa amemfahamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli kabla hajawa Rais wa Tanzania.

Akizungumza na Azam News, Polepole amesema kuwa Rais huyo ni msikivu anasikiliza ushauri kwenye vikao anaacha wajumbe waseme kisha yeye anasikiliza hoja ambayo wajumbe wanataka.

“Mimi nimemfahamu Rais Magufuli kabla hajawa Rais wa Tanzania, nimemfahamu akiwa Waziri nimemfahamu akiwa anatafuta kugombea CCM akapewa dhamana kwenye kampeni amekuwa kiongozi wangu kwenye serikali na sasa ni kiongozi wangu kwenye chama na sasa ni kiongozi wetu wa nchi kama ni mtu mmoja namfahamu ni msikivu anasikiliza ushauri mnapokaa kwenye vikao mnaacha wajumbe waseme kisha yeye atasikiliza hoja kwa kwenda ile ambayo wajumbe wanataka ni Magufuli sasa mtu unapokwenda kutoa kauli ya kumaliza mjadala kwamba huyu hasikilizi ushauri tenda haki uwe mwanifu hata kufa Mungu wetu wa mbinguni atakupa taji ya uzima,” alisema Polepole.

Aidha Polepole alizungumzia baadhi ya viongozi wa dini kuzungumzia siasa alisema “Viongozi wetu wa dini wanahudumumia Mungu na watu wake kauli kamilishi isiyokuwa na ushahidi ni kitu kibaya ukisema huyu mbona amekamatwa kwa mambo mabaya amekamatwa kwasababu ni mhalifu anatuhumiwa kwa uhalifu katoa lugha ya kichochezi, Tanzania, Marekani mpaka China ukitoa lugha ya uchochezi ni kosa la jinai na anaekushtaki siop Rais ni kwa mujibu wa sheria na ni jamhuri inayokushtaki wewe.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents