Burudani

Nimepigiwa tu simu, simjui mtu yeyote kwenye hilo tamasha la Nigeria – Vanessa Mdee

Sina shaka tayari umeshafahamu kuwa muimbaji Vanessa “Vee Money” Mdee amepewa mualiko wa kwenda kutumbuiza kwenye tamasha kubwa la ‘Gidi Culture Festival’ nchini Nigeria, ambalo Vee amesema waandaaji walimtafuta wenyewe.

Vee Money-2

Vanessa anaamini kuwa juhudi zake za kuutangaza muziki wake kimataifa ndio zimefanya waandaaji wa tamasha hilo la ufukweni, kuona kuwa kwa Tanzania yeye ndiye msanii anayestahili kuwa miongoni mwa wasanii wakubwa wa Afrika kama Awilo Longomba, Iyanya na wengine walioko kwenye orodha ya watakaotumbuiza (Ingia hapa).

“Nadhani kutokana na vile tunapigana na kuupaiza muziki wa kizazi kipya wa Kitanzania” Vanessa aliiambia Amplifaya ya Clouds Fm. “Nimepigiwa tu simu, simjui mtu yeyote kwenye hiyo festival na wala sina connection yoyote, nimefanya tu kupigiwa tu sina na nilichoambiwa ni kwamba namba yangu walipewa na Leslie Kasumba ambaye alikuwa boss wa Channel O.”

Vee n K.O

Vanessa ambaye wiki ijayo ataachia wimbo mpya aliomshirikisha rapper mkali wa Afrika Kusini, K.O ameongeza kuwa amepata nafasi ya kusafiri na madancer wake kwenye tamasha la ‘Gidi Culture Festival’ litakalofanyika April 4, 2015 Lagos, Nigeria.

“Tumejiandaa ipasavyo nimepata bahati ya kwenda na madancer wangu so itakuwa show kubwa sana” alisema babe wa Jux.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Vee Money kutumbuiza kwenye show kubwa Nigeria, lakini safari hii akiwa amepewa heshima kama wasanii wengine watakaotumbuiza siku hiyo kwasababu amepewa mualiko rasmi na waandaaji wenyewe.

December 15, 2013 Vee Money alikuwa msanii pekee wa Tanzania aliyepata nafasi ya kutumbuiza japo kwa dakika tano tu, kwenye tamasha lingine kubwa la ‘Harp Rhythm Unplugged’ ambalo lilifanyika Lagos, (Ingia Hapa) lakini hii ilikuwa ni kutokana na connection za Vanessa na meneja wake Abby.

Vanessa Afrima

Mwishoni mwa mwaka jana Vee Money pia aliongeza thamani yake kama msanii kimataifa baada ya kushinda kipengele cha ‘Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki’ kwenye tuzo za AFRIMA zilizotolewa Lagos, Nigeria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents