Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Nina jina kubwa tofauti na kipato – Dully Sykes

Msanii wa muziki Bongo, Dully Sykes amefunguka sababu ya kutosimamia wasanii kwa sasa tofauti na hapo awali.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma ‘Bombardier’ ameiambia The Base, ITV kutofanya hivyo kunatokana na kipato kuwa kidogo licha ya kuwa msanii mwenye jina kubwa.

“Ilisimama kwa sababu hata kipato hakikuwa kikubwa, mimi siyo msanii labda mwenye kipato kikubwa, nina jina kubwa tofauti na kipato, kwa hiyo siwezi kusema jina langu lina uwezo wa kumchukua msanii no!!, nilitakiwa nipate kipato kwanza ndio nianze kumsimamia msanii wangu” amesema Dully Sykes.

Hata hivyo Dully ameongeza kuwa kwa sasa ana wasanii wawili tayari ambao ndio anataka aanze nao rasmi ingawa anajua anapoanza na msanii lazima kipato kidogo kiwepo kwa ajili ya kufanyia video, production nzuri na kusukuma wimbo (production).

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW