Burudani

Nina miaka 32 najiona nimekua, najutia sana kuchora tattoo na kutoboa masikio-Mr. Blue (+video)

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Mr Blue amesema kuwa anajutia sana baadhi ya vitu ambavyo alishawahi kuvifanya kipindi cha nyuma akiwa mdogo ambavyo hadi sasa vinamuumiza kichwa.

Akitaja baadhi ya vitu hivyo kwenye mahojiano yake na Bongo5,  Mr. Blue amesema kuwa ni kitendo cha kutoboa sikio akiwa darasa la 7 na kuchora tattoo.

Kwa upande mwingine amewaasa wasanii wengine hususani wachanga kutokufanya vitu ambavyo baadae vitawaletea majuto kwani kila fasheni inabadilika kuendana na muda.

Related Articles

46 Comments

  1. Tatizo watu hawaelewi ,,ukiwa msanii kuna vile inatakiwa uishi ili kuonekana tofauti na wengine ,,na vile inatakiwa uishi ndo kama hivi kutoboa pua na kuvaa hereni kutoboa masikio na kuvaa heren kuvaa vikuku kuvaa nguo aina zote za kike za kiume kuchora tatoo,,,kupaka lipstic shedo ,,,kupaka wanja ya make up kiujulma ,,,hivyo ndivyo msanii apaswa aishi kwa life style yake yote

  2. Ndiyo Nassour Barrack Kheir na ndiyo maana wasanii wengi Africa hawaonekan kufanya mambo makubwa au kupata dili kubwa kama wale wa america kwa sababu wasanii wetu Africa hawajui ku ji brand yani unakuwa auwezi kutofautisha msanii na muuza nyanya barabarani

  3. Neah Pike acha uwongo. Jay Z hana tattoo hata moja, hajatoboa sikio hata moja, miongoni mwa wasanii matajiri duniani nae yumo. Unataka kuniambia pesa ameziokota hajazipata kupitia usanii? Acha kukariri ndugu, ubaweza kuwa msanii bila kuchora tattoo, kutoboa sikio ama pua na pia ukawa na mafanikio maana mafanikio ya usanii hayaangalii tattoo zako wala hereni zako wala vikuku

  4. Nassour Barrack Kheir yani wale jamaa ujui wanavyo ji brand kuna mambo mengi wanafanya ata kama hawajitengezi miili baadhi yao ila kuna jinsi wanajitengeneza wewe huwezi jua ,, ila sina maana kwamba asilimia mia kuji brand nilikoongelea Mimi ndo kunawafanya wale wa America kuwa na mafanikio makubwa noo wale kuna mengi mfano wana uhuru wa kuimba wanachoona wanachojisikia pia lugha yao ni kimataifa pia taifa lao kubwa lina maendeleo

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents