Burudani

Nina mtu kwenye team yangu kazi yake ni kunitafutia miwani kali – Dogo Janja

Msanii Dogo Janja amesema kuwa ni vibaya msanii kuvaa nguo zinazofanana na shabiki wake na iwapo wakifanana, basi shabiki awe amepata nguo hiyo kwa tabu.

Dogo Janja

Dogo Janja amekiambia kipindi cha Ladhaa 3600 cha E Fm kuwa msanii ni kioo, hatakiwi kuenda jukwaani kuimba alafu wanakuja watu kama wanne kumshangilia alafu wawe wamevaa kama yeye

“Ni vibaya sana na haitakiwa, unatakiwa uwe tofauti sana na uwe mbunifu kuchagua nguo. Sio shabiki tu mtu yeyote, bbora shabiki avae kama wewe ila hicho kitu akipate kwa tabu, si anajua hizi tisheti zinauzwa sh. 13,000 Kariakoo.

Ameongeza kuwa kinachompa kiburi kusema hivyo ni kwamba nguo zake huwa anaangiza kutoka nje ambazo huja kwa kupimwa uzito na si kama vijana wengine.

“Hamna msaanii anayevaa au mwenye muonekano wa kistaa kama mimi East Africa, naamanisha ninachokisema, mimi kwanza hadi kuniona hivi nina watu ambao wamenizunguka. Nina team kubwa ya watu imenizunguka kushughulika na muonekano wangu, hiyo ni nje ya management, mpaka miwani nina mtu ambaye anahusika nayo.

“Mimi huwa sataki kuongea bei, nawatiaga watoto hasira ili wakatafute alafu wanakosa wanaishia kunitukana, hawapendi hasa mabishoo kwa sababu vitu ninavyoweka hawavikuti sehemu kwa hiyo wanapaniki. Hata cheni ninayovaa huwezi kuipata hivi hivi, nywele yangu tu ina gharama ya msosi wao wa siku, yaani ina gharama kama ndevu za Rick Ross,” amesema Dogo Janja.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents