Habari

Ninabana kwa mafisadi ninalegeza kwa masikini – Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa alichaguliwa na watu masikini hivyo ni lazima awe upande wa watu masikini huku akisema kuwa anabana kwa mafisadi ana legeza masikini.

Kauli hiyo ya Rais Magufuli ameitoa jana mkoani Kagera wakati wa ufunguzi wa mradi wa wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba, mkoani Kagera ambapo amesema kuwa kuna meli mpya ambayo inakuja hivyo wananchi wa Kagera wajipange kwaajili ya kufanya biashara.

“Uchumi haujengwi bila kuwasaidia wajenga uchumi, ukisafirisha ndizi kwa kupitia barabara ya lami kuzunguka kule gharama ni kubwa nilazima wasafiri kupitia hapa, kwahiyo kwenye mwezi wa 12 au mwezi wa kwanza mwanzo tunasaini mkataba tunasema ukweli kwasababu msema kweli mpenzi wa Mungu siwezi nikasimama hapa mbele yenu nikaanza kuzungumza uongo ninajua nitahukumiwa nikisema uongo nataka nisihukumiwe kwa hili nataka dhambi zangu nikasamehewe kwa kusema ukweli hata kama unauma kwahiyo Meli inakuja, lakini si meli mpya tu na meli ya MV Butiama tunazi karabati upya nataka meli ziwe zinapishana hapa nataka watu wafanye biashara,” alisema Rais Magufuli

“Ninabana huku mafisadi nina legeza kwa wananchi masikini , nina bana kwa mafisadi ninalegeza kwa watu masikini, nilichaguliwa na masikini nilazima niwe upande wa masikini, ninataka niyazungumze haya kwasababu nimepata nafsi ya kuzungumza nimesikia hapa Bukoba ukibeba ndizi hapa unatoa ushuru ninajua hii halashauri hii ni ya Chadema lakini mimi ni Rais wa Watanzania wote, Mkulima yoyote atatozwa ushuru atakapo pakia zaidi ya tani 1,” aliongeza Rais Magufuli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents